Scroll to Top

#Indundi film| Filamu hii “ALAUMIWE NANI”?, imeteng’nezwa na The King’s Club Film kutoka Rumonge

By La Rédaction / Published on Monday, 09 May 2016 01:18 AM / /

ALAUMIWE NANI

Je, mapenzi yanaweza kuwa kikwazo katika familia ?

Vijana machachari kutoka kundi linalojulikana kwa jina la « THE KING’S CLUB FILM » kutoka RUMONGE wanawaletea filamu mpya « ALAUMIWE NANI »? part 1&2.

Ni filamu ya kisasa yenye kufunza jinsi gani binadamu wanaweza kuishi kwa amani na upendo na majilani.

Hadhisi yake ni kijana mmoja alikuwa anaishi kijijini alafu akadumbukia ndani ya mapenzi na binti mmoja ila kaka wake binti hakufurahia mapenzi yao ndio maana akaanza kutafuta njia ya kuhalibu mapenzi yao.

Alipotekeleza vizuri aliona kwamba ni lahisi kumuagiza dada wake katika familia iliokuwa mjini.

Kisa na mkasa binti ametimua kuishi mjini alafu mpenzi wake akabakia kijijini. Siku chache kadha, kijana yule amepata fulsa ya kwenda mjini kufanya kazi  akapakuta binti mzuri mtoto wa boss wake na wakaanza mapenzi kighafla.

Baada ya wiki chache, Boss akagunduwa kwamba pesa zilizopo kwenye akaunti yake zimegawanyika na akakumbuka kuwa ni yeye na mtoto wake wa kike tu wanaoruhusiwa kutowa pesa kwenye akaunti yake sasa akaanza upelelezi ili ajuwe pesa zilipotelea wapi. Kijana wetu sasa akaanza kupata taabu hadi ya kuwaga dunia.

Fatilia kisasi hiki ili upate kujuwa mengi zaidiiiii !

USIKOSEE, IKO  MADUKANI !!!

181 total views, 0 views today

Add Comment