homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesRurebeyaswahili

Simon Mashakado na kazi mpya

Kijana Simon Mashakado mwenye kabila ya kikongo ila mwanafunzi nchini Burundi, kwasasa anaendelea kufanya vizuri kwenye swala nzima la kuinuwa Tasnia ya Filamu sasa Baada yakutengeneza Movie nyingi kwasasa amekuja na TUNDA LANGU ambayo ni Movie yenye kujaa Mapenzi, Manyanyaso pia na Kilio

Movie hio ikiwa inaongelea:
Alikuwepo kijana ambaye anaitwa Gema amekuwa na uusiano wa kimapenzi na dada anayeitwa Sarah, Kweli walipendana sana, ila kutokana naukosefu wa kijana Gema basi familiya ya Sarah ikamuowesha Sarah kwa mwanaume mwengine anaeitwa kwa Jina la Vita. Ila Sarah katika ndoa yake ameishi maisha ya shida sana mumewe Vita amekuwa akimunyanyasa sana, Gema amesikia kuumizwa sana na mateso anaoyaishi Sarah, Gema hakuchoka kumufatilia Sarah nakumuambiya kama bado anaitaji kuwa naye maisiano ya kimapenzi kama zamani, Ila Sarah amekuwa akimwambia Gema kama haiwezekani tena maana tayari ameishakuwa mke wa mtu, atakama Sarah amekuwa akiteswa ila amekuwa muvumilivu wa ndoa yake.

Alivyo ongea na Indundi saizi vijana hao wamesema kuwa movie hio baada ya mwezi itaenda kuachiliwa nakuwapa mashabiki wake kazi mpya na uku akiwaahidi kuwa nikazi yenye uwezo na acting ya juu zaidi

Indundi TV inamtakia mafanikio makubwa kwa kijana huo. Je unamshauri nini?

What's your reaction?

Related Posts

1 of 291