homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Vincent Kigosi : “Mimi ni mkongwe, mtu wa zamani”

Amenyoosha maelezo kuhusu watoto ambao anataka kuwa nao katika familia pamoja na kutumia ukongwe wake katika kazi zake.

Vincent kigosi Ray baada ya kuulizwa kuhusu kukaa kimya kwa muda mrefu : “Mimi ni mkongwe mtu wa zamani,hata mambo yangu nitayachanganya kizamani na kisasa ili nipate kitu kikubwa katika soko la filamu la Tanzania, sijaonekana siku nyingi lakini nakuja sasa,sisi ni watu wazamani naangaliaga tulikosea wapi na tunatakiwa kuelekea wapi”
Ameendelea kueleza kuwa ana kitu kikubwa anakifanya kinakuja kuanzia mwezi wa Oktoba mwanzoni au mwishoni ambapo ataangalia ratiba yake itakavyo kuwa kabla ya mwaka huu ahujaisha

Pia ameeleza kuhusu mpango wa kuongeza watoto wengine ambapo amesema kila kitu ni mipango ya Mungu,hata mtoto hawakupanga kuzaa ila imetokea ikawa hivyo,ila anategemea kupata watoto wa wili tu anafunga kazi.

Hata hivyo Ray amesema ana mpango wa kuachia filamu itakayohusu maisha yake na familia kuanzia mtoto wake na mama mtoto huyo Chuchu Hansy

What's your reaction?

Related Posts

1 of 246