Vijana wengi wanaojishuulisha na sanaa ya uhigizaji nchini Burundi wanazidi kutowa malalamiko yao kuhusu kukosa msaada wowote kwa wadhamini wa Filamu ili kuweza kuendelesha kazi mbele.
Indundi.com imeweza kukaa na wasanii wakongwe nchini nakuwauliza nini tatizo : “Burundi yetu tunaipenda na pia tunaitaji Pia tuanze kuwakilisha nchi yetu kimataifa kupitia filamu kama jinsi tunaona Tanzania, Kenya na Nigeria, ivi ni kwanini filamu zetu hazitazamwi kwenye nchi hizo? sio kwamba tunashindwa tunaitaji sapoti kubwa ili kuakikisha kazi zinatoka na ubora kwanza sisi tunaigiza vizuri sana ila cha ajabu ata location tunanyimwa sasa watu wengine wataijuwa aje nchi yetu kama ni nzuri kipindi kila movie hadi kijijini, nasio eti story azipo ni nyingi sana ila ata nyumba mtu ananyimwa kazi zitakuwa aje nzuri”?
Walimaliza kwa kutowa maoni yao basi Indundi ikauliza nini ifanyike ili kazi ziende kimataifa :
“Sisi tunaomba sana kwanza sio serekali tunaitaji matajiri wakubwa na wenye ma company waweze kutusaidia maana iyi kazi ya filamu nikama biashara ukiwekeza vizuri namkatafuta soko lazima matunda mtayaona, kwa hiyo tunaitaji msaada kutoka kwenu naamini tunaweza”.
Walimaliza kwa maombi ayo ,pia kabisa inasikitisha sana kwa vijana wanavyo jitowa kweli wanastaili msaada ikiwa wewe una uwezo saidia vijana maana nikama kusaidia nchi.