homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Mfahamu vizuri kijana muigizaji “Mathématique”

Kijana aitwae Mucowintore Saidi maarufu kama Mathématique kupitia jina analotumia kwenye kazi yake ya Comedy leo ameeleza kuhusu alivyo anza kazi yake ya Filamu pia na comedy

“Majina kamili naitwa Mucowintore Saidi ila nafaamika kwa jina la kazi “Mathématique” ni muigizaji wa movie na comedies pia na mtunzi ama (muandishi).

Kuigiza nilianza zamani sana tangu nipo shule za chekechea nipo miongoni mwa wanafunzi ambao nilikua sikosi stejini kwa sherehe za kila siku za masomo. So mambo ya kuigiza nilianza ningaliki na umri mdogo sana”. Alisema Mathematique.

Pia alipo ulizwa nizipi changamoto alizo pitia amejibu :
“Changamoto ambazo nakumbana nazo haswa katika hii kazi kwanza nyuma wazazi wangu walikua hawapendi kabisa mimi kufanya hiki ambacho leo nafanya ,so kwangu hiyo ndo ilikua changamoto kubwa sana kwangu ila kwasasa wameshaanza elewa taratibu kutokana na utendaji wangu wa kazi, na nimesha bahatika kunyakua tunzo moja tu tangu nianze safari yangu hiyi ya sanaa nje ya nchi ambapo ilikua nchini Rwanda kwenye tunzo za A THOUSAND HILLS ACADEMY AWARDS edition2 nilibahatika kupata tunzo ya best upcoming actor mwaka 2014-2015”. Aliongea Mathematique.

Pia alimaliza na ahadi kwa mashabiki kwamba:
“Nitapambana na kuakikisha nawapa kazi zenye ubora wa hali ya juu na filam za kwetu kufaamika zaidi Africa na dunia nzima”.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 288