Msanii wa filamu nchini Burundi Djuma Mababi afaamikae kwa jina la Jay, baada ya yeye kufanya Filamu ya FIKRA iliyo zinduliwa mwaka huu mwezi wa Aprili chini ya Company ya Filamu TGF inayofanyia kazi Kamenge, kijana huo Jay amesema kwamba kwa sasa anajipanga kwa ajili yakufanya kazi kubwa sana ila anacho kitazama nikwamba anaitaji alete mapinduzi tofauti na Filamu yake aliocheza Fikra.
Alipo ulizwa ni kwanini, amejibu :
“Tatizo naikaa naona wasanii wengi nchini Burundi pia na wa producer wanashindwa kuwa wabunifu kwenye hii game ya Filamu na ndio maana siku kwa siku tunashindwa kuendelea sasa mimi nataka kuandaa filamu ambayo itakuja kuleta mabadiliko makubwa sana kwenye Tasnia yetu na nitatumia uwezo mkubwa wa kuigiza ili niweze kurizisha mashabiki wangu maana naitaji kujijengea mashabiki wangu kwanza na pia niwarizishe maana bila wao sioni kama mimi naweza kufikia malengo ambayo nilio nayo”. Alisema Jay Mababi
Kijana huo Jay Mababi ameshiriki kwenye Filamu nyingi na ajafikia kufanya kazi akasimama kama Actor Principal ila unapotazama Acting yake ni kubwa sana na yenye uwezo.
Basi Indundi Film kwa ilivyo na hamu yakuona Vijana wanaendelea basi tunamtakia mafanikio mema kwenye kazi yake