homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Msanii wa Filamu Tanzania na ujio mpya nchini Burundi

Msanii Frederick Habona Michael ambae ni muigizaji nchini Tanzania na ameweza kutengeneza Filamu inayoitwa CAPTAIN HABONA alioachia mwaka jana na imetambulishwa na Comapny ya marehemu Steven Charles Kanumba iitwayo KANUMBA THE GREAT FILMS, kijana huo ambae anaonesha uwezo mkubwa wa kuigiza nchini Tanzania na kujitolea umaarufu mkubwa sana apo na uku akishirikiana na mzazi wa kike wa Steven Kanumba ambae ni FLORA MTEGOA ,uku akiendelea na kazi nyingi ambazo zitakuja kimataifa na utofauti mkubwa.

Mwaka 2018 kijana huo Habona amekuwa Burundi kwa njia yakuja kutazama jinsi Industry ya Filamu apa Burundi inaviokwenda na ameweza kukutana na wasanii pia na producer Wise Pro na wameongea mengi.

Ila baada ya Indundi Film kumuona tena mahali hapa nakumuuliza alichokuja kuandaa badala ya kuja Burundi mwaka jana na ivi anarudi tena, alijibu :

“Mimi kwanza kama nimekuwa hapa mwaka jana nimejifunza mengi sana kuhusu waigizaji wa Burundi na pia nimeipenda sana nchi hii kwa io niliporudi Tanzania nimejifunza kwanini nisifanyi Movie kubwa apa itakayoleta utofauti mkubwa basi nimekaa chini na Crew nzima ya HABONA FILMS Pia nikishirikiana na KANUMBA THE GREAT FILMS nikaweka project mezani na kwa sasa nipo hapa Burundi siwezi kusema nini nakuja kufanya ila napenda tu niwajulishe kwamba project hii mtaona na mtapenda, maana ata movie yangu ya CAPTAIN HABONA niko naandaa kuachia pia kwa warundi ndugu zetu waweze kuona pia”. Alisema Habona

Kweli tunaamini kwamba Burundi pia vipaji vimeanza kuonekana na matarajio ya Indundi Film ni kuja kusaidia wasanii pia ikiwa na wewe ni msanii waitaji maendeleo yako jitaidi sana kujongelea indundi Film maana kwa pamoja tutafika.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 511