homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Cameramana & Editor wa Filamu za Burundi akiwaponda wa Cameramen fake wanaoharibu kazi

Minani Mussa maarufu kama Mo Mussa ambae ni kijana anaejituma kwenye kazi ya ku shoot movie pia na kufanya Editing, amezifanya kazi nyingi kwa kujituma na kuweza kusaidia vijana wengi kwa kupiga hatuwa ikiwa kama companya ya Bekiss pia na zingine nyingi sana.

Baada ya Indundi kusikia malalamiko ya waigizaji wengi kulalamikia wa Cameramen wengi kwa kuwaaribia kazi, basi tuliamuwa kumtafuta umoja wa wacameramen nchini Burundi natulikutana na kijana aitwae Mo Mussa na tulipo muuliza anasema aje kuhusu malalamiko haya, amejibu:

“Unajuwa kwanza wasanii peke yao ndo hawajuwi maana ya kazi hii na kama inatokea wanakosa sapoti sababu hizo niwao wenyewe kwa sababu hawajuwi kutafautisha Cameraman yaani wanamkuta tu mtu kwasababu anayo camera maramoja anataka wa shoot Movie, kumbukeni kuwa Cameraman wa harusi hawezi shoot movie maana hii Movie inatakiwa mafunzo kwanza mtu akaelekezwa na sio kukurupuka tu”.

Basi Indundi tulimuuliza swali la mwisho kinacho takiwa nini ili wafikie malemgo, alisema:

“Mimi ninachoweza kuwashauri wajikaze sana watafute ma nyumba makubwa ya Production kama PAPY JAMAICA, CONGRADEC, STUDIO TANGANYIKA, na wengine wengi pia wajitowe wasibani pesa ili wapate kazi nzuri zitakazo wafikisha kimataifa na sio wakae nafikiria kutengeneza Movie zakuishia ndani kwao tu ,lazima mubadilike sisitupo kwa ajili yenu”. Alimalizia Mo Mussa.

Kwa iyo Wasanii waigizaji wa filamu jitaidini sana kuamka tofauti na leo amkeni mapigeni atuwa maana filamu ikija kukosa Quality nzuri na Sound ikawa nzuri filamu yako ahiwezi kutobowa kimataifa.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 191