homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Nduwimana Ninette Déborah, muigizaji aliyejichukulia umaarufu kwenye Filamu aja na mapya

Muigizaji NDUWIMANA Ninette anaejulikana kwa jina Déborah ambae ameshiriki kwenye hiyo Filamu ya DEBORAH na amejichukulia umaarufu mkubwa kwenye Tasnia ya Filamu akiwa bado mdogo, alivyoanza nakufikiria kuwa ni jambo la kawaida tu ila baada ya filamu hiyo kutoka watu walitamani kumuona kwa vituko alivyovifanya ndani ya Filamu, kwa sasa amekuwa na umri mkubwa na kuja na ujio mpya wa kazi ambayo ameshirikishwa na msanii kutoka Tanzania ambae anajulikana kwa jina ya CAPTAIN HABONA ,Baada yakugunduwa mtoto huyo anakipaji kikubwa sana.

Basi indundi tumejaribu kumtafuta na tukamuuliza kwanini aliamuwa kukaa kimya mda mrefu, alisema: “Mimi baada ya Filamu yangu ya DEBORAH sio kwamba nimekosa wakunitafuta ili nishiriki kwenye movie zao walikuwa wengi tu ila wazazi wangu baada yakuona umaarufu umekuwa mwingi kwangu wameogopa kwamba nikiendelesha kazi hii nitashindwa na masomo maana kipindi hicho nilikuwa bado mdogo, ila kwa sasa namshukuru Mungu wazazi wameniruhusu na apo nilipo sema tu kwamba nataka kurudi kwenye game yangu ndipo nikakutanishwa na Capatain Habona na nikajitowa kufanya kazi pamoja.
Ila mashabiki wangu kitu kimoja tu niseme ni kwamba mashabiki wangu wakae tayari maana nimeona upendo wao tu kipindi niko na shoot wamejaa wengi kunitazama na awakuamini kuwa nimimi nimekuwa kiasi hiki ila niwaambie tu nawapenda sana”. Alimaliza Deborah

Ikumbukwe kuwa huyu ni binti mwenye uwezo mkubwa sana wa kuigiza kwa hiyo tusubiri mazuri kutoka kwake na tuzidi kuwasapoti vijana wetu.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 185