homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Aimablue : Mimi ni msanii wa Filamu anaejielewa pia nakuja upya

Aima Blue msanii wa filamu aliye jichukulia umaarufu mkubwa mwaka 2017 kwenye filamu yake ya MISSED CALL na ameweza kutumia wasanii wakubwa pia wenye uwezo na kuweza kupata nafasi kupita kwenye Interview mbali mbali za radio hadi na Television, na kwasasa ameweza kuwa kimya mda mrefu sana ila ujio wake ni wa kasi.

Basi akiwa ndani ya Studio ya INDUNDI TV aliulizwa nini chanzo cha yeye kuwa kimya mda mrefu alijibu: “Kweli nimekaa kimya mda mrefu tokea kipindi nilipo towa filamu ya MISSED CALL na ilitokana na matatizo binafsi ya maisha na ikiwemo pia kukaa nakujifunza nini nitafanya baadae ,kweli nimekaa na nikajifunza yote ayo na kwa sasa nimeamuwa kurudi kwenye game na utofauti mkubwa ambao sintokuja kulala tena na kwa sasa nakuja na Filamu yangu mpya iitwayo LYNCA Naaamini filamu hii itakuja kuwa tofauti sana na msangao pia kwa mashabiki tena kitu nikumbushe ni kwamba watu wajitowe kutusaidia na sisi mfano kama Indundi Tv inavyo fanya kweli nasisi tunaitaji pia tuone tunafika mbali na nyinyi ndo wakutufikisha mbali”.

Aima Blue amemalizia nakusema :I”ndundi Tv nitakuwa pamoja nanyi pia nawajivunia sana. Vijana wa Burundi malalamiko yao nikwamba wanaitaji sapoti mbali mbali zitakazo wawezesha wao kupiga hatuwa kubwa sana na wanaimani watafika tu maana wenye wamefika mbali leo hawashindi chochote bali uwezo tu.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 511