homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Happy River : Najiamini sana kwenye filamu za Kirundi na watu wanazipenda sana

Kijana Happy River maarufu kama RIVER ni kijana anaye jituma sana kwa kazi zake apa nchini Burundi na anafanya movie ambazo zimeanza kukubalika ndani na nje nakujichukulia umaarufu mkubwa ,vile ikumbukwe kuwa pia ni cameraman na editor na baada yakufanya kazi nyingi ndani ya studio ya IMPANO VIDEO na kazi zake kusikika hadi Tanzania na ndipo ameweza kupata mkataba na kiongozi wa HABONA FILMS COMPANY ambae kwa sasa yuko apa nchini Burundi nawakiwa wanafanya kazi pamoja.

Baada ya INDUNDI TV kumuuliza nini anacho kiandaa upande wake River amejibu kwamba:

“Kwanza niseme nina mengi sana yakuachia mwaka huu maana baada yakuwa kimya kwenye soko ya filamu haijamaanisha kuwa nimekuwa kimya kuandaa movie apana, nimesha andaa movie nyingi ila ambayo naitaji kwa sasa ingie sokoni na sio kuingia ki ivi ivi tu bali nataka nifanye uzinduzi mkubwa sana hio filamu inaitwa UBUZIMA kabisa ni filamu ambayo nimetumia uwezo mkubwa sana kabisa kuanza pre-production hadi Production na pia nimeweza kushirikiana na company ya JC PRODUCTION na pia naitaji kabisa ije ifuraishe mashabiki wangu pia naomba sana Indundi Tv iweze kutusaidia kwa upande mwengine ili kazi zetu zije kufika mbali”. Alimaliza River.

River ni kijana mwenye kujituma sana na mwenye uwezo mkubwa maana ni yeye baada yakuona tasnia ya filamu za kirundi kuzima alionesha ushujaa na filamu zake kuonyeshwa ma television tofauti apa kwetu na kupendwa na watu kiasi kikubwa, kweli nyumani kuna vipaji vikubwa sana vya kusaidiwa kwa kweli.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 194