homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Hastar Danger, msanii wa filamu kutoka jijini Rumonge aonekana kwenye kazi za Bujumbura

 

Msanii wa Filamu ajulikanae kwa jina la Hastar mkaazi wa Rumonge ila kwa sasa akiwa ameanza kutumikia kazi zake apa Bujumbura,pia nikijana ambaye amejichukulia umaarufu mkubwa kupitia Filamu ambayo ameitowa apo Rumonge iitwayo IBAKI STORY na kuonekana kuwa msanii wa kiume ambae anagingiza jiji ilo la Rumonge katika kupita kwetu nakusaka vipaji tumeweza kukutana na Hastar Bujumbura na tukauliza vipi kuhusu kazi yake, Hastar alijibu:

“Kwanza niseme namshukuru Mungu sana kwa kuwa kipaji alicho kiweka ndani yangu ni kikubwa sana na nikitu ambacho siwezi kupoteza kwa kweli ,na kwasasa nipo Apa Bujumbura na ninaendelea na kazi kama kawaida ndani ya Company ya TAMBWE THE GREAT FILMS na verry soon tu mtaanza kuona kazi zangu zinawajia tena kwa kasi zaidi labda nitowe shukrani kubwa sana kwa wasanii wenzangu wa Jiji la Rumonge pia na kwenye kundi langu la RFU ambalo limenifanya hadi niwe Actor mkubwa kiasi ichi na kupendwa na watu, naamini mambo yatakuwa mazuri na nitaakikisha apa bujumbura naiwakilisha vema Jiji langu”, Alimaliza Hastar.

Kweli tukumbuke kuwa nchi ya Burundi ni kubwa na Rumonge pia ni moja ya sehemu ya Burundi na kuna vijana ambao wanajituma na wanajuwa nini wanacho kifanya,kikubwa ni kupenda vya kwetu na kuvisapoti pia naamini tutafika tu pamoja na Mungu

What's your reaction?

Related Posts

1 of 193