homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Abema Charles, msanii kutoka Congo akiwa Burundi kutazama wasanii wake

Msanii afaamikae kwa jina la Abema Charles Kiongozi wa Company ya AC Company ambae anaishi Congo ila ameweza kufanikisha kuezeka Company yake nchini Burundi nakupata wasanii wazuri wenye uwezo mkubwa wa kuigiza ameonekana akiwa Burundi na kujumuika pamoja na wasanii wake kwa kazi mbali mbali, basi na ameweza kueleza kikubwa kilicho mleta Burundi

Abema kwenye ukurasa wake wa Facebook amesema kwamba:

“Kwanza nashukuru sana Mungu kwa kuniwezesha hadi sasa nazidi kuona Company yangu ya AC Company Burundi linaendelea kusimama imara na pia najivunia sana wasanii wangu wanao jitowa kwa kazi,pia Lengo kubwa lakufika Burundi ni ajili ya ukaguzi pia nakupata Ripoti kubwa ya Company toka miezi mi wili kuanzishwa na Kubwa zaidi ni ajili ya Production ya filamu mpya am bayo Soon tu tutaanza kazi,na kweli nimefurahi kwanza nimekuta wasanii wako salama na wote wapo kwenye Mood ya kazi kweli napenda sana wasanii wangu na napenda sana Burundi” .Aliongea Abema

Muonekano wa maendeleo ya Filamu Burundi inazidi kuendelea na vijana wanaonekana kweli kuipenda kazi yao na kuleta mawasiliano mazuri kati ya nchi kwa nchi, kweli Burundi itaonekana na kutambulika kimataifa kwa nguvu za vijana ambazo wanakuja nazo tofauti na mwaka jana.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 511