homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Bizimana Hafsa, Mama anaezidi kuonesha bidii yake kwenye kazi za filamu za kiswahili

 

Bizimana Hafsa maarufu kama Mama Hafsa kwa sasa anazidi kuonekana kwenye kazi tofauti za filamu na akiwa anaonesha uwezo wake wa kuigiza nakuanza kujijengea mashabiki tofauti kila kona,na anaoneka kuwa mwenye kujituma maana ukitazama sana kwa upande wa wakina mama niwachache sana ambao wanajituma kuigiza basi tuliona ni vizuri sana tumtafute na kukaa naye tujuwe ni kitu gani kilicho sababisha hadi yeye aanze kazi hio ya Filamu.

Mama Hafsa ameongea:

“Kwanza mimi hii kazi ya kuigiza nilikuwa naipenda toka zamani sana ila nimekuwa nikisikia abibu maana kipindi hicho kwenye filamu nyingi Burundi wamama watu wazima walikuwa hawajiingiza kwenye sanaa ndo nikasema kwamba sasa kwenye watu wazima hawapo kweli siwatanicheka ila baada ya hapo nimekaa kwanza siku moja kuna rafiki yangu alikuwa anaigiza ndo nikamwambia tu kwamba namimi anipeleke basi alipo nifikisha hapo Director wangu aliona kwamba nina uwezo mkubwa sana wa kuigiza na ndipo akaniamini nakunipa nafasi kwenye Movie walioipa jina la “PAIN OF LOVE”. Nilicheza kama Doctor na nimeweza kuakikisha nafasi yangu naitendea haki baadae nimeshiriki kwenye filamu inaitwa BARAKA, pia nikacheza ShortFilm ya NABII MRUNDI na ivi kuna mpya karibuni itatoka inaitwa ZINDUKA, kweli namshukuru sana Director wangu Tambwe na anazidi kunipogisha atuwa niseme tu kwamba nitawafurahisha ma funs wangu hadi wajiisi raha”. Alimaliza mama Hafsa uku akichekaa.

Kweli Tasnia ya Filamu Burundi ikianza kuonekana ndani watu wakubwa itakuwa vizuri sana nakuleta maendeleo makubwa. Mfano ukitazama filamu za Tanzania watu wanajitowa kiukweli ,kila kazi ukiishika kama kazi lazima ikupe eshima kubwa baadae.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 191