homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Tambwe akionekana na utofauti ndani ya filamu “Zinduka”

Muigizaji na mtunzi wa Filamu nchini Burundi maarufu kama Tambwe kwa sasa ni kijana anaejitafutia umaarufu kwa hali ya juu pia nakutafuta maendeleo ya kazi zake nchini Burundi na anazidi kuonekana mpya kila siku kwa washabiki wake kwa kuwaletea kazi za kibunifu siku kwa siku, na hadi kijana huo kujichukulia unaarufu mkubwa katika mtandao wake wa Facebook pale anapotowa tangazo yakuwa anakwenda kuachia kazi mpya na mashabiki wake kuonesha hamu kubwa yakusubiri kazi hio. Kutokana na hayo, Indundi Films imeweza kumtafuta nakukaa naye chini nakutaka kujuwa utendaji wake wa kazi unatokana na nani?

Tambwe amesema :

“Mimi kwanza hapa ni ukosefu wa Management tu maana nina hamu ya kufanya ubunifu wa hali ya juu kabisa tofauti na huu wanao uona hapa maana kwanza mimi najielewa sana na pia nina ndoto yakuinuwa tasnia ya nyumbani iweze kusikika kimataifa na naamini ipo siku japo mda haujafika ila naomba wa Manager warundi waliopo ndani ya Burundi ata na wale ambao wako nje please waweze kutusaidia ili tuweze kufika mbali maana bila wao sisi turabiki kila siku ivi tu, kwa ihyo naomba pia Serikali ituunge mkono kwa kweli”.

Ikumbukwe kuwa Tambwe ameanza kuonesha njia kubwa ya mafanikio ya kazi hii maana kila kukicha kijana huu tunamuona akifanya kazi bila kuchoka wala kukata tamaa pia kutokana na changamoto anazo kutana nazo ila yeye anasimama tu, kweli kijana huu nimfano wakuigwa ata kwa waigizaji wengine maana tasnia ya filamu Burundi bila ubunifu hatuwezi kufika.
Basi amkeni kwa pamoja na mtaweza pia upendo na amani vikitawa ndani yenu.

Indundi Films pamoja nanyi !!!

What's your reaction?

Related Posts

1 of 287