homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Balufutu ni muigizaji wa filamu upande wa comedy anaongea kuwa yeye ni namba moja

Muigizaji wa comedy aitwaye kwa jina la Wabenga Augustin maarufu kama Balufutu mchekeshaji maarufu kwenye Tasnia nzima ya Filamu kweli nikijana mwenye kujituma sana na kuonekana kupendwa kwenye ma show tofauti alizokuwa anazifanya na Generencha Bidondo pande za birimani, na kwasasa anakuja kivingine na kusema kwamba anataka atumike ili aanze kurizisha wasanii wake kila mda na anaimani kuwa mambo yatakuwa mazuri sana na kingine anasema kwamba Management sio shida ila anaamini kupitia kazi zake lazima management ikuje tu.

Basi alipo ulizwa na Indundi kwanini amekua ameacha Balufutu alisema:

“Mimi nimekuwa nimeacha Comedy kutokana na changamoto furani ambazo zimekuwa zikijitokeza kipindi nikiwa nafanya Show ya Comedy pamoja na management ya Generencha ila nimeamuwa kutulia nakujifunza nini nianze kufanya na kwasasa kweli nimefanya karibu miaka miwili sipo kwenye game na nimekaa nikajifunza mambo mengi sana ila naamini ninavyo rudi nitakuja tofauti sana na watu wanavyo nizowea mimi Balufutu, pia niseme kwamba hapa sijaona Comedian wakunitisha mimi maana wote bado wa underground na najikubali wakitaka wakatae ila naamini mimi nakuja kuwa number moja”. Alimaliza Balufutu

Yaani ukitazama sasa kwenye tasnia ya comedy kweli imeanza kuleta changamoto kwa wasanii na wote kukataa number mbili kila mtu akijisifu kuwa yeye ni number moja na wote wakitowa ahadi kuwa wanakwenda kuleta mabadiliko makubwa kwenye tasnia ya filamu kabisa Mungu azidi kuwabariki nakuwapa nguvu ya ubunifu mkubwa pia indundi Tv iko kwa ajili yenu nakuwatafutia maendeleo ya vipaji vyenu ili muweze kufikia ndoto zenu.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 517