homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Fidy, muigizaji wa filamu nchini Burundi na sura mpya ya kazi

 

Fidy ni muigizaji wa filamu za kiswahili nchini Burundi ila kwa sasa anaishi nchini Rwanda na ndipo anapo fanyia kazi yake ya sanaa.

Hapa Burundi alianza kuigiza kwenye kundi la BAHO ambalo Director alikuwa anaitwa Madja na aliweza kubahatika kucheza kwenye filamu tofauti na alipo badirisha makao na kwenda kuishi Rwanda ameendeleza pia nakushiriki kwenye filamu na alicheza kama mrundi.

Indundi Tv ilipo muuliza nini malengo yake na mipango yake, Fidy alisema:

“Mimi kwanza najiamini kwenye kazi yangu na ndo sababu kubwa sana yamimi kuto kukata tamaa ya kucheza na kwa sasa niko nakuja Burundi kuna filamu nakuja kushiriki pia nakuja kujiunga na Company ya Filamu hapo Burundi ila sitotaaja jina la Company hio ila naamini wataona kazi na ndo watajuwa kweli nimekuwa nimekosekana sana kwenye tasnia ya Filamu hapo Burundi ila kwa sasa niahidi watu wanao nijuwa na wasio nijuwa kwa sasa nakuja kivingine sana na malengo yakuinuwa filamu za Burundi”.

Wasanii wa Burundi wanashindwa kukata tamaa maana siku baada ya siku waigizaji wanaendelea kujituma kila pande ili kuweza kukamilisha malengo ambayo walionayo nakuinuwa nchi kimataifa

What's your reaction?

Related Posts

1 of 191