homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Zuzu, msanii wa kike nchini Burundi anaekuja na utofauti mkubwa sana kwenye tasnia ya filamu

 

 

Zuzu muigizaji wa filamu Burundi aliy tamba kwa kazi tofauti hadi kufikia kiwango cha kushirikishwa kwenye filamu ya MIUJIZA ambayo imesimamiwa na mkurugenzi wa company ya ESHIMA VIDEOZ Baada ya apo alipata nafasi ya kushiriki kwenye filamu ya Dude na Patcho Mwamba ambayo imetengenezwa nchini Tanzania aliweza kujichukulia umaarufu mkubwa sana na pia alivyo fika Rwanda ndipo amefanya filamu nyingine.

Basi alipo ulizwa na indundi Zuzu amesema:

“Mimi kwasasa nataka kuja tena kwenye game na kazi nzuri pia kwa sasa naishi Rwanda na nimefanya kazi hapa na Mungu akasaidia kwenye Association za Filamu Rwanda pia na mimi nashirikishwa na baada ya kukaa mda mrefu bila kuwa chini ya uongozi wowote kuhusu Filamu kwa sasa nimeamuwa kurudi nyumbani nakuja kujisajili kwenye Company ya filamu badae nitumike na watu waone kazi zangu. Pia ni wakumbushe mashabiki wangu mwamba wapende sana vya nyumbani na watowe sapoti zao kwetu ili tuweze kufika mbali filamu za Burundi zitabadilishwa na waigizaji ikiwa waigizaji watajituma kama tunavyoona maana mabadiliko ya sanaa yanaletwa na wana sanaa, na wanawake wa Burundi wameanza kujitowa nakujituma kwenye tasnia ya Filamu kweli lazima mabadiliko yaonekane”.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 194