homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Tambwe Remy na ujio wa kazi yake mpya yenye muonekano tofauti

Kijana Tambwe ambae kwa sasa anaonekana sana na kazi kubwa sana kwenye Game ya Filamu nchini Burundi siku baada ya siku anazidi kuonekana kwenye mitandao ya kijamii na kazi zake mpya apo ni Baada ya Tambwe kucheza Short Film ya NABII MRUNDI na ZINDUKA na baadae ku Producer ShortFilm iitwayo KIPOFU na alikuwa kama Director tu kwa sasa ameonekana na ujio wa kazi mpya iitwayo THE SHOCK ambayo anasema ataachia siku za usoni apa.

Indundi Tv ilivyo mtafuta amesema kwamba :

“Kwanza mimi Filamu hii naichukulia kama kazi na mda mwingi sana mimi ni mtu najituma sana, kusema waigizaji wakubwa kama marehemu Kanumba na Vincent Kigosi waitambulishe nchi yao ya Tanzania kimataifa walitumika sana tena vyakutosha kabisa na walikuwa siyo watu wakukata tamaa kama tunavyo sikia Interviews zao, ndio maana na mimi nasema kwamba sitochoka kupambana maana najuwa baada ya siku mambo yatakuwa mazuri kweli kweli na sisi tutaona njia ya mafanikio. Kwa sasa najipanga kuachia kazi moja iitwayo THE SHOCK na najuwa imejaa mashauri mengi sana na itakuwa nafaida kubwa kwa watu. Kwa hio mashabiki wangu wajipe moyo kwamba mimi Tambwe nitaiwakilisha vema nchi yetu” Alimaliza Tambwe

Kweli Tambwe nikijana mwenye umri mdogo ila mwenye bidii kubwa na moyo wakutokukata tamaa, anazidi kuwakilisha vizuri wenzake kabisa vijana wanaitaji msaada kutoka kwa wadhamini pia na kwa serikali ili waweze kufika malengo yao na ndoto zakuinuwa nchi kimataifa kupitia Filamu.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 246