5.5 C
New York
Thursday, October 28, 2021
HomeCECAFA Challenge cupRose Ndauka aweka wazi picha za mwanaume aliempost wakiwa pamoja

Rose Ndauka aweka wazi picha za mwanaume aliempost wakiwa pamoja

 

Muigizaji wa filamu za kibongo, Rose Ndauka amefunguka kuhusiana na mwanaume aliyempost ikisadikiwa kuwa ni kibenten (mwanaume anaelea) wake, kuhusu mwanaume anayemtaka na kuumizwa kwenye mapenzi bila kusahau habari za baba wa mtoto wake.

Kuhusu habari ya Kibenten, Rose Ndauka ameieleza EATV & EA Radio Digital, baada ya kupost picha katika mtandao wake wa Instagram na kuandika kuwa yupo na Kibenten.

“Unajua Instagram kuna watu vitu wanapenda na niliandika vile nilijua watu watatiririka tu, lakini sio kweli yule ni mdogo wangu tu, niliandika kuwa nipo na ‘kiben…. whaaat’ ila watu wamejieleza lakini sikuwa nimeweka wazi ila nilijua akili ya watanzania watasema nini” – Rose Ndauka

Aidha Rose Ndauka ameendelea kusema hawezi kuwa na mahusiano na Kibenten na hajaona sababu ya kuwa na Kibenten ila alishawahi kuumizwa kwenye mapenzi na alichukulia kama funzo.

Pia amesema anapenda kuwa na mwanaume mchapakazi anayependa familia aliyekamilika na hamtaki mwanaume anayelala kitandani tu.

Kuhusu habari za kumficha baba wa mtoto wake, Rose Ndauka amesema sio mbaya kama yeye pekee akimjua mtoto wake na baba wa mtoto inatosha licha ya watu kudai kuwa wametengana na mzazi mwenziye na hatoi malezi kwa mtoto ndiyo maana hamuonyeshi.

- Advertisment -

Must Read

SAT-B ngo yasabwe gukora arekane n’abavuga gusa

0
Abantu bahanuye Sat-b gukora gusumba kwishinga abavuga, ivyo bikaba bishikirijwe ku rubuga rwiwe Aho yariko amenyesha abantu ko Imana ariyo yamukuye mu bworo. uwo muririmvyi...