BurundiCECAFA Challenge cuphomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Happy River anashituwa tasnia ya filamu kwa kazi yake mpya

Kijana Happy River ambae ni msimamizi wa Company yake iitwayo HOT RIVER FILMS, River ni kijana anae endelea kujituma na kutumika sana uku akiamini ipo siku atakuja kuleta mapinduzi ya sanaa, apa jana tumeona ame post picha nyingi akiwa mwenye kufunga ndoa ila chakushangaza tulipo muuliza ametujibu kuwa iyo ni Filamu na hajfunga ndoa na tumemuuliza kuhusu gharama zote ili afikie kuitimiza ili ikamilike.

Basi amejibu River:

“Kwanza niseme jambo mimi nashukuru sana kuona nyinyi watangazaji mnaanza kutusapoti mda wote nakutujali jambo nalotaka kusema ni ivi mimi nimetumika sana Filamu za kirundi pia kweli zimenipa jina baada ya kazi zangu kuangaliwa na watu wengi sana ila baada ya apo nimekaa nakufikiria nini nifanye ili nije kuleta utofautu mkubwa kwenye Industry yetu ya filamu, nimekaa na timu yangu nzima ya River Hot Film nikawafikishia wazo langu na hawakupinga wamekuwa bega kwa bega na mimi hadi tukafanikisha basi ndo tupo tunaliandaa ili bomu ambalo tutalipuwa mda usiokuwa mrefu maana sisi tunaamini tulicho kipanga ni kitu kikubwa zaidi, pia washabiki wangu wasijali wazidi kuniamini kama wanavyo niamini tu kila siku ila kupitia mzigo huu lazima wakubali tu nakuona mabadiliko kwenye kazi zetu”. Alimaliza River.

Umoja wa maendeleo na ubunifu wa kazi nilazima wasanii watafikia malengo yao…Mungu awabariki.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 543