BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

“Nitasimamia haki ya Buja movie na kufanya chochote hadi nihakikishe saana ya Burundi imeinuka”

Muigizaji wa filamu nchini Burundi maarufu kama Mulove ni mtu mwenye kuonekana na bidii sana kwenye kazi yake ya kuigiza pia ametembea sehemu tofauti ili kutafuta maendeleo ya filamu Burundi, na baada ya yote anacho kiandaa nikusema kwamba anaitaji kutumika kazi nzuri zitakazo wafikia mashabiki wake na wakafurahi.

Basi alipo ulizwa na Indundi nini malengo yake amesema Mulove: “Malengo yangu mimi siyo yangu tu bali malengo yangu yapo kwa Taifa nzima kuakikisha tunafika mbali sote kwa pamoja ikiwa mimi na waigizaji wenzangu pia na Burundi nzima tuweze kuitambulisha kimataifa na pia ilo naamini litawezekana tu maana kazi tunayoyifanya ni kazi kubwa sana labda niseme tu kwamba mimi nimejifunza mengi nimekuta East Africa na sisi Burundi tunaweza sana ila wasanii wanashindwa kujielewa inatubidi tuweke nguvu kwa pamoja na naamini tutafika tu maana akuna kitu kizuri kinacho kuja bila umoja na kwasasa niwajulishe wale wanaonijuwa na wasio nijuwa kwamba ninakuja kitofauti mwaka huu nitaakikisha mambo yanakuwa sawa na nitafanya Filamu za ubora zitakazo wafuraisha nyote kwa ujumla kimoja tu tambuweni kwamba nawapenda na nipo apa ajili yenu. Burundi ni nchi yetu natunaipambania ili kufikia malengo”. Alimaliza ivo.

Kweli waigizaji wakiweka nguvu yao kwa pamoja lazima watafika nakuleta mabadiliko makubwa sana kwenye tasnia ya filamu.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 536