BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Muigizaji wa filamu « Jolie » na muonekano mpya kwenye tasnia ya filamu Burundi

Muigizaji wa filamu nchini Burundi Jolie kwasasa aja naujio mpya kwenye filamu nchini Burundi baada ya kukaa mda mrefu akiwa kimya pia ni muigizaji aliye shiriki kwenye filamu nyingi sana na mwaka jana aliweza kutengeneza filamu iitwayo KAFARA aliyo ifanyia mkoani Rumonge na filamu hio iliweza kushiriki wasanii wakubwa wa tasnia ya filamu nchini Burundi pia Jolie ni mwanamke mwenye kujituma  sana kwenye tasnia pia INDUNDI TV tumeweza kumtafuta nakuongea naye na tumemuuliza nini anacho kipanga kwa mwaka huu aliweza kutowa maelezo nakusema :

“Mimi ni mrundi pia najivunia kuwa mrundi na niko hapa ajili yakupigania nchi yangu kuitangaza kimataifa kupitia filamu na kutokana na ilo jambo kubwa ambalo limesababisha mimi kuingia kwenye filamu ni kwasababu nimekuwa nikiona mda mwingi sana filamu za kitanzania na apo nimeona sana wanawake wenzangu wakisimama na kupambana ajili ya filamu pia walipata jina nchini kwetu na ndipo nimesema kwamba inatubidi na mimi kusimama ili kupambania filamu zetu maana filamu pia zinaitaji wanawake wazuri ili iwe namuonekano mzuri”.

“Na ninacho weza kusema ni kwamba mimi huu mwaka wa 2020 nakuja kivingine kabisa kuakikisha kipaji changu kinapanda zaidi ili kuakikisha nchi jirani wananijuwa pia naitakji Mungu anisaidie ili niweza kuleta tunzo nyumbani kwetu kama vile Natacha anavyo fanya”. Alimaliza ivo.

Inavyo onekana kama ahadi zilizo tolewa na wasanii wa filamu nchini kwamba mwaka huu ni mwaka ambao watageuza tasnia ya filamu nchini Burundi nakuipandisha kwa level nyingine, basi kwa sura hii tunaamini kwamba Mungu atakuja saidia maana wasanii ni wenye kujituma pia nawenye kujielewa tofauti na mwanzo.

Indundi Tv inawatakia maendeleo mema.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 544