BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Muigizaji na Mchekeshaji Samba Famba atarajia kuachia kazi mpya

Msanii FAMBA SAMBA muigizaji wa filamu kwenye secta ya comedy ni kijana anae jituma kwa sana baada tu ya mda mrefu sana kutoonekana kwenye management yake ya Team Pro ambayo inasimamiwa na DJ Pro, Samba alikuwa ni Msanii mwenye kujituma sana ila pia alikuwa na ndoto ya kuwa muimbaji kabla ya filamu. Basi indundi ilivyo mtembelea aliamuwa kujiweka wazi nakusema :

“Mimi nimezaliwa Rugombo ni Actor wa Comedy pia naimba, ila sana sana ndoto yangu ilikuwa nije kuwa muimbaji mkubwa kwenye Buja Flever maana tokea nipo mdogo nimependa sana kuimba nakufatilia music kwa makini ila nilipo kuwa na miaka 8 nilikuwa nikichekesha watu kwa kuongea kwangu ndipo waliona kwamba nina uwezo wakuchekesha watu, basi nikaanza kuchekesha nikaona sifa zimepanda zaidi ndio nikaanza kuwa mchekeshaji ila huku nikitamani kuimba hadi leo baadhi ya ndoto zangu kutimia.”

SAMBA aliongeza :

“Mimi mwaka huu nakuja kivingine kabisa maana tunaitaji kuinuwa tasnia yetu ili iweze kufika mbali na yote ndo mwaka huu lazima tuyatimize, pia mashabiki wangu jiandaeni kupokea kazi zangu”.

Kweli FAMBA SAMBA baada ya kuwa mchekeshaji tunazidi kupata nyimbo zake siku kwa siku na anaonekana mwenye kipaji kweli, vijana kujituma ndo njia ya maendeleo.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 198