homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Jojo Rashmy : wasanii wa kike Burundi tuamke tufanye kazi kwa bidii na siyo kujivuna

Muigizaji wa filamu nchini Burundi JOJO RASHMY mwenye uwezo mkubwa wakuigiza filamu kwa scene yoyote ile kwa maelezo yake pia ameshiriki kwenye filamu ambazo zimefanya vizuri apa na inje hadi kupata nafasi kubwa ya kushiriki kwenye SERIES ambayo inaandaliwa inchini Tanzania pia ameweza kushiriki kwenye filamu iitwayo KAFARA Na apo scene zake kupendeza zaidi na producer hadi kumpelekea kushiriki filamu iliyo andaliwa na company ya UKEBURWATANS na kushika CERTIFICATE OF BEST ACTRESS, ila baada ya kukutana na indundi tv tukaweza kumuuliza kutokana na neno alilo sema kwamba wanawake waigizaji wa Burundi wameikalia majivuno kuliko kufanya kazi amejibu :

JOJO RASHMY:

“Tatizo wasanii wetu ukiwaambia ukweli wanakuona vibaya kabisa na kipindi unawaonesha ukweli ili waweze kujirudia ndani japokuwa wanaweza kuwa na ndoto zakuwa kama Wema Sepetu ao Aunty Ezekiel, wasifikirii kwamba ni kawaida wale walijitengeneza vya kutosha kabisa hadi wafikiye ivo ndo maana naweza kusema kwamba inabidi nasisi tuache majivuno ya kijinga ili tuweze kufikia ndoto zetu ,tusibaki kuwa watu wakuvutiwa na wengine ila tujikaze na sisi kesho ao kesho yake tuanze kutazamwa  na kuwa vivutio kwa wengine. Kinacho nishangaza mimi leo unaona msanii ametengeneza movie mpya baadae anakuwa kimya nakuachana na kundi lake hadi aanze kutafutwa kweli uyo si ujinga mkubwa ninacho weza kuwaambia ili tupate pesa lazima kwanza tujenge majina kila sehemu maana filamu ni biashara inayo itaji jina kwanza ,pia atuwezi kupata sapoti kwa njia iyo.”

Alimaliza Rashmy

Filamu ni biashara ambayo inaingiza pesa kupitia na vile kazi ilivyo kwa iyo kimoja ni kwamba wasanii wa Burundi wakijituma sana lazima watafika mbali maana wameanza kuelewa kitu ambacho walikuwa hawajuwi na kinasababisha wao kurudi nyuma zaidi na kujiona kama hawawezi kabisa ila watangazaji wakiwa sapoti lazima wafike mbali.

Weka maoni yako chini…

What's your reaction?

Related Posts

1 of 195