BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Joy Amuri : Mimi ni msanii mpya kwenye tasnia ila naitaji kuwa zaidi ya star maana wengi hawajielewi

Muigizaji wa filamu JOY AMURI ni msanii mpya mwenye kujituma zaidi kwenye filamu japokuwa ni mpya sana ila tumeweza kuona baadhi ya filamu zake na moja iliyo fanya vizuri inaitwa KISANGA ambayo imeweza kumpa umaarufu mkubwa zaidi na baada ya apo kuonekana tena akiwa kwenye shooting ya filamu nyingine mpya ambayo inasemekana kwamba ivi karibuni itaanziwa matangazo basi tulimuuliza kwanini anasema kwamba wasanii waliyo mtanguliya hawajielewi Joy alisema

JOY AMURI:

“Kwanza kubwa zaidi kinacho nishangaza wasanii wa nyumbani ni kwamba wanapo fanya kazi moja ao mbili mara moja wanaona kama wamemaliza nakuanza kujiita ma star, mimi kweli jambo ilo linakuwa linaniuzi sana tena sana kwa upande mwengine hadi wanakuwa wanatuzarahu sisi wanyuma kumbe wanashindwa kuelewa kwamba kuwa star nikazi ya kujitengeneza kwa njia zote nzuri na siyo kwa kujivuna ,kwanza mimi kiubinafsi nina ndoto yakuwa star mkubwa na sio star wa Burundi tu hadi nje ya nchi lazima niakikishe ilo ndo kwa maana nasema kwamba huu mwaka lazima nione nusu ya ustar ,nitafanya kazi yoyote ile ili mradi tu nije nitokelezee na kupata eshima maana naamini ipo siku raisi wetu atanipa pongezi kwa nguvu nitakazo tumia mimi kijana wake, pia kitu kingine nitapendelea kuambia wasanii wenzangu tuwe na moyo wakupendana na tuache majivuno ili tuweze kuweka nguvu kwa pamoja kuakikisha tunafikisha nchi yetu mbali, pia neno la mwisho ni kwamba na mueshimu sana Director wangu na company linalo nifanya mimi kuwa star wa baadae.

Alimaliza Joy…

Kweli JOY alieleza maelezo yake kwa uchungu mkubwa zaidi na kuonesha mara ngapi anatamani inchi yake iwe ya kwanza EAST AFRICA kwenye maswala ya Sanaa ,kweli kiupande mwengine ni kwamba Burundi ya sasa siyo kama ya zamani ki filamu maana ivi kweli kuna mabadiliko makubwa sana.

Towa maoni yako pamoja na indundi tv…

What's your reaction?

Related Posts

1 of 198