BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Papy Bienms : Waigizaji wa filamu wengine hawajielewi ajili hawana ndoto

Muigizaji wa filamu Papy Bienms ni msanii anaezidi kufanya vizuri kutokana na kipaji chake na kuanza kutafutwa kila sehemu kama mshiriki, na katika kazi zake ya moja iliyo mtowa inaitwa ARDHI YA CHOKWE.

Basi tumeweza kuwasiliana naye nakumuuliza kwanini waigizaji wengine hawana ndoto kama alivyo sema, basi amejibu :

“Kweli waigizaji wengi wa filamu nchini Burundi hawana ndoto maana kwanza ndoto zimetofautiana kuna ile ndoto mtu anaota kitandani End of the day akiamka basi ila kuna ile ndoto nyingine mtu anakuwa ameota akiwa kwenye kipaji chake sasa iyo ya kipaji ndo ninayo ongelea mimi unakuta wasanii tupo wengi ila hakuna faida yoyote Ile zaidi ya kila msanii akijiona bora anatamani afunguwe tu Group nayeye ili mradi akuwe Kiongozi ao Director kinacho takiwa kwanza Burundi tupunguze ujuwaji kabisa maana ndo kitu kinacho sababisha sisi sanaa yetu ahifiki mbali wala akuna maendeleo yoyote ile, kweli Burundi sisi tunaweza sana kabisa ila tatizo kubwa ni ilo wasanii tuwe na ndoto kwenye vipaji vyetu tuweze kuinuwa tasnia yetu maana ni furaha sana kwangu kesho ao kesho yake Burundi tunakuwa tunaitwa Kimataifa tukienda kushiriki kwenye Movie kubwa kubwa, na neno langu la mwisho niseme kwamba watu wataona ndoto yangu mwaka huu”. Alimaliza uku alicheka.

Kweli muigizaji akiwa na ndoto yakufikia jambo lazima alifikiye ,kubwa zaidi ni kwamba wasanii wa Burundi wajitume sana kwa ilo ili kuweza kubadilisha filamu za nyumbani.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 198