homepageIndundi CinemakirundiMoviesswahili

Simon Mashakado : “Nimetowa ahadi ya kubadili tasnia lazima niitimize”

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi Simon Mashakado ambae anazidi kujituma siku kwa siku ajili aweze kutimiza kile kitu ambacho ame ahidi kwa washabiki wake mwaka huu,tumegunduwa baadhi ya pic zake akiwa ana shoot basi tumemuuliza ni ujio gani. Basi amejibu Indundi kwa furaha akisema :

“Kwanza nakumbuka siku yangu ya mwisho nafanya Interview na Indundi nimesema kwamba mwaka 2020 nitafanya mambo makubwa na nikatowa ahadi kabisa basi kama ilivyo ahadi ni deni lazima nitumize ndo maana upande wangu naweza kusema kwamba huu mwaka nakuja na utofauti mkubwa sana kwenye Tasnia ya Filamu pia niseme tu kwamba baada ya ile Filamu yangu ya SOFIANA kwa sasa nakuja na nyingine kali zaidi japo sintoweza kusema title ila ni Filamu ya mila ya zamani kwa hio ninacho weza kusema ni kwamba watu wangu wajiandae kupokea mambo mazuri kutoka kwangu na mtafurahi sana kwa kweli sina mengi ila zaidi tuwe pamoja na sapoti zenu bado naziitaji.”

Kweli Simon Mashakado ni kijana anaye zidi kujituma bila kukata tamaa ya mafanikio na kila siku mvumilivu hula mbivu basi kila la kheri na Mungu azidi kukubariki.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 581