homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Gad : “Mwaka huu lazima nifanye filamu kubwa ya kimataifa”

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi Mr Gad mwenye makao yake makuu mkoani Rumonge ,ni muigizaji ambaye anaendelea kujituma sana siku kwa siku na kazi zake kuendelea kufanya vizuri sana nchini Burundi apo ni Baada ya kijana huo kufanya Filamu ya KIJIJI CHA UCHAWI na ikaweza kukubalika Rumonge hapo ni baada ya Mr Gad kuja kwenye Indundi nakuuliziwa Plan yake ya huu mwaka Gad amesema :

“Kusema ukweli nina wengi na mengi ya kushukuru sana kupitiya kipaji changu maana kwanza moja Serekali na viongozi wa Rumonge wanazidi kutusapoti sana na kutuleteya maendeleo vijana wao pia tunazidi kujituma na sisi kwa ujumla nakupambana ili katika mikoa ya Burundi Rumonge ije itokelezee kuwa ya kwanza ki Filamu, na kuhusu kwanza Mimi Nina kundi yangu inaitwa THE KINGS CLUB na mimi ndo Kiongozi pia mwaka huu Kufanya Filamu kubwa na wasanii wa inje lazima zifanyike maana ata na sisi tuna iyo plan yakufanya kazi mpya ambayo itakuja kuwa surprise kwa washabiki wangu na warundi pia kwa ujumla,Kweli Naamini mwaka wa 2020 ni mwaka ambao tunakimbizana na kutafuta tunzo inje ya inchi ili kuleta eshima kupitia Sanaa”.

Rumonge ni kati ya mikoani iliyopo Burundi na nimoja ambayo ina  wasanii ambao wanaigiza Filamu kwa lugha ya kiswahili na kazi zao kuonekana hadi Bujumbura ,Kweli Burundi ni inchi yenye maendeleo kwa upande wa vijana Mungu azidi kubariki vijana wetu wa Burundi na maendeleo yao ,

Na sapoti zinaitajika ili kuwasaidia zifike mbali zaidi na zaidi.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 517