homepageIndundi CinemaMovies

Nemcy le Madame : “Nimefanya kazi mingi sana ambazo zinakubalika”

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi Nemcy A.k.a Le Madame ni mwana dada ambaye anazidi kujituma sana kwenye kazi zake nakuzidi kuonekana na utofauti mkubwa sana na amezidi kuonesha uwezo mkubwa wa uchezaji na kushiriki kwenye Filamu nyingi sana zenye muonekano mkubwa sana. Basi alipo kutana na Indundi amejieleza na kusema kwamba :

“Moja kwanza I am so happy kuwa muigizaji pia na ivunia kuwa mrundi nakuishi Burundi pia watu wanaweza kujiuliza kwanini najiita Le Madame kwanza moja nijiamini sana kwa kipaji changu na nazidi Kufanya vizuri siku kwa siku na kweli mwaka huu nimeweza kushiriki kwenye Filamu nyingi sana tofauti na yote ni kwasababu najipeleka vizuri kwenye maigizo na siyo tu ivo kwanza msanii anastaili awe mtu mwenye eshima na nidhamu kwa iyo upande wangu mimi nasema kwamba kweli Mungu amenijalia. Na lingine niseme kwamba huu mwaka lazima nitatumika hadi nje ya nchi niitwe maana kwa sasa nimeanza kuona njia niseme tu kwamba Mungu yuko pamoja na sisi ,pia sasa ivi niko chini ya Uhongozi wa TGF Company na ndipo nimeanza kufanyia kazi zangu Soon tu apa wataanza kuona kazi mpya kwa iyo washabiki wangu nawapenda sana kabisa na wakae kwenye mkao wa kula”.

Burundi ni nchi ambayo kwa sasa inaongoza kwa wasanii ambao wanazo ndoto zakuitambulisha nje, kwa hio Mungu awajalie na kama malalamiko yao yalivyo kwamba wa naitaji sana sapoti kutoka kwa Serekali.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 185