homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Hii ndo sababu yake kuamuwa kwenda na kukaa katika nchi ya Congo

Muigizaji wa filamu nchini Burundi ajulikanae kwa jina la Sadiki Henry ni muigizaji pia anahusika na utafutaji wa soko za filamu nchini Burundi hapo ni baada ya kwenda kukaa katika nchi ya Congo, kwa kurudi aliweza kukutana na Indundi Tv na kusema :

“Kweli Burundi yetu ukitazama kwa sasa tupo nyuma sana kuhusu soko la Filamu yaani nimeona kabisa ni tofauti sana na zingine nchi ambazo ni jirani yetu. Kweli baada yakuwa Burundi kwa mda nimeamuwa kwenda kwanza Inchini Congo ajili yakutafuta njia yakuweza kuuza Movie zetu kwanza nilicho kiona kule watu wanapenda sana kazi zao tofauti na sisi ,kumbe tunacho takiwa tufanya sisi nikupenda kwamza Kazi zetu wenyewe na wasanii kuondosha zile Bifu za kupumbavu. Na kitu kingine ni kwamba tujitaidi kufanya kazi nzuri zenye mafunzo maana sasa ivi jamii inatuangalia sisi kama wasanii nini tufanye na nini ya msingi ili tufikiye malengo kumbe kubwa zaidi ni wasanii tubadilike pia wadhamini wasiogope kuweka pesa yao kwetu maana kazi ni ivo lazima tujitume kwa sana kabisa ili tuweze kufika mbali na sisi kama wasanii tunawaakikishia kwamba tutafanya vizuri maana nimeona ata inje ya Burundi kazi zetu zinapendwa kwa iyo uwezo unakuwa mdogo sana kabisa ndio maana napendelea kusema kwamba watuone ili tufanye vizuri zaidi.” Alimaliza Henry.

Kweli uwezo ndo kitu kinacho wakosea waigizaji wa Filamu kutoendelea nakushindwa kufanya kazi zao kumbe inabidi wadhamini wasimame nakuunga mkono ao kuwekeza pesa kwa tasnia ya Filamu Burundi

Nini maoni yako?

What's your reaction?

Related Posts

1 of 518