homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Tambwe Remy na movie mpya akimshirikisha mama Kanumba

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi HAKIZIMANA REMY maarufu kama Mr Tambwe baada yakufanya kazi nyingi sana nakuonekana mwenye kupambania Tasnia ya Filamu Burundi kwa njia nyingi tofauti ya maendeleo basi ni baada ya kuonekana kwenye Cover akiwa pamoja na Mama Kanumba ndipo aliulizwa swali na Indundi kuhusu hio kazi na alisema :

“Hii ni ndoto nilioibeba takribani miaka mi 5 sasa maana ndoto yangu mimi imekuwa kufanya Movie na marehemu Steven Charles Kanumba ila kwa bahati mbaya akafariki ila baada ya hapo nikaanza kumuona mama Kanumba kwenye game ndipo nikaamuwa sasa kuanza kumtafuta mama Kanumba kweli imekuwa vigumu hadi nilipo kuja kumpata ndipo nikaanza kuzungumza naye na tukaanza kupanga kazi ila mda tulio upanga haikuwezekana ajili ya uwezo imekuwa shida sana kwangu kabisa ila Mungu amejalia katika upambanaji pamoja na Team yangu tumejitaidi sana hadi tukafanikisha ku shoot uku nayeye aka shoot Tanzania na baadae tu movie itatoka. Pia sio hio kazi tu ila kuna mengine mengi mazuri ambayo nayaanda, ni siri zipo kubwa sana ila moja tu washabiki wangu wajuwe kwamba huu mwaka ni mwaka wa mabadiliko makubwa sana lazima nije na utofauti mkubwa sana.” Alimaliza Tambwe

Ikumbukwe kuwa kijana huu Tambwe anazidi kujituma sana kwenye sanaa ya nyumbani pia ni kijana mwenye kutafuta soko kila kukicha ,Burundi ni nchi yenye vijana wanao jielewa kutokana na vipaji vyao. Mungu azidi kuwabariki.

Towa maoni yako…

What's your reaction?

Related Posts

1 of 511