homepageIndundi CinemaMoviesswahili

The Brothers company : Uzinduzi wa movie hii itakuwa moto

Company ya utengenezaji na uandaji wa Filamu nchini Burundi The Brothers Company ambayo inazidi Kufanya vizuri siku kwa siku na kuleta utofauti mkubwa sana kwenye Tasnia ya Filamu nchini Burundi na kuzidi kuitangaza sana ya Filamu. Hapo ni Baada ya kutengeneza Filamu mpya iitwayo IRONDO na kufanya Tour za uzinduI kila sehemu sasa ni zamu ya Bujumbura kwenye Hotel kubwa ya MARTHA HOTEL.

Baada ya kuwasiliana na mkurugenzi wa Company hio ametueleza akisema :

«Kweli tunafanya vile kama tulivyo ahidi mashabiki wetu kwamba mwaka huu wa 2020 lazima tulete mabadiliko makubwa sana kwenye Tasnia na kuzidi kuwapa kazi nzuri na tumeweza kutowa fursa hii kwa mashabiki ikiwa kwamba hujapata nafasi kwenye uzinduzi uliyo pita basi hii ni yakwako tutakuwepo pale MARTHA HOTEL.

Na itakuwa tarehe 22 mwezi huu na kiingilio ni pesa 20.000 tu ,kwa msaada tunaomba mashabiki wetu na pia wasanii wenzetu bila kusahau wapenzi wa Filamu za Burundi tunaitaji mje kwa wingi maana bila nyinyi sisi hatuna maendeleo kabisa. »

Basi ili ni kwa wale wanao towa malalamiko kwamba Burundi hakuna Filamu basi tukutane sote MARTHA HOTEL kwa kutowa sapoti.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 246