homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Jaclus : “Kama nilivyiosema 2020 ni mwaka wa ushindi kwa kila msanii”

Msanii wa filamu nchini Burundi bwana Jaclus ambae anazidi kujituma sana siku kwa siku na kazi zake na ni mkurugenzi pia wa kundi lake binafsi BMC kwa urefu “BEST MOVIE COLLECTION “, kijana huo anazidi kuonekana na utofauti mkubwa sana kwenye Industry nzima ya Filamu nchini Burundi.

Baada ya kuonekana baadhi ya mapicha akiwa location tumewasiliana naye na tukamuuliza kuhusu kazi hio amefunguka akisema :

“Kweli Filamu is My Job na pia naipenda sana. Kusema ukweli mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko makubwa sana na ni mwaka wa kila msanii kuwa mshindi kutokana na ndoto zake. Niseme tu kwamba mimi kuna kazi niko na andaa ila sinto sema mambo mengi sana ila kwa mtazamo tu tegemeeni kazi kubwa ambayo inakuja mda si mrefu maana nimejifunza mengi kwa miaka iliyo pita nikaja kugunduwa kwamba kweli sijafanyaga kazi ivi sasa ndo nataka kutengeneza Filamu na jambo moja nitaomba kusema kwa warundi muweze kutusapoti vijana wenu ili tufike mbali kweli maana tuna ndoto zakuinuwa nchi yetu kimataifa kupitia Filamu.

Na lingine ni kwamba mwaka huu lazima tulete tunzo nje maana Filamu zetu zinakuja na ubora wa hali ya juu, tumejifunza nini inaitajika kwenye Filamu ili iwe bora, kwa hio washabiki wetu mjiandae kupata Filamu nzuri na yenye kueneza kila sheria ya kuitwa Filamu.” Alimaliza JACLUS.

Filamu ni njia yakutambulisha nchi yetu kimataifa kwa hiyo ikiwa sapoti zitaonekana kwa vijana wetu lazima watafikisha nchi mbali kupitia sanaa.

Towa maoni yako…

What's your reaction?

Related Posts

1 of 284