homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Herment Rich: Filamu Burundi inalipa ila sisi hatujielewi

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi kwa jina la Herment Rich maarufu kama Mr H, ni kijana ambaye anajituma sana na mwenye muonekano mzuri kwenye Performance yake na anajielewa sana kwa utendaji kazi wake ,na pia ni kijana ambaye ameshashiriki kwenye Filamu nyingi tofauti sana na kuonesha uwezo wake mkubwa sana na kufurahisha kila mtu. Baada ya maojiano yake na Indundi Tv, tumeweza kumuuliza  swali kwanini anasema kwamba Filamu inalipa na kipindi wasanii wenzake wanalia kwa ajili ya soko alisema :

“Kusema ukweli ni kwamba Filamu ya Burundi ni kweli inalipa ila kiasi kikubwa cha wasanii wanashindwa kujielewa ninapo sema jambo kama awajielewi namaanisha kwamba tunakuwa tukifanya kazi za kitoto sana yaani wasanii Atujielewi pia nikichangia ata kwa wa Director inabidi mujifunze namna yakuweka sawa wasanii kwa upangaji wa casting maana iyo itatusaidiana sana kabisa kuinuwa Tasnia yetu ya Filamu na Kuweza kuifikisha mbali kwa iyo niseme tu kweli tukiishika sanaa yetu kwa mikono miwili lazima tufike mbali.” Alimaliza Herment

Kweli kila kitu kinakuwaga na thamani yake pindi utakapo tambuwa kuwa kina umuhimu kwa iyo sanaa ya Burundi kweli inaweza kulipa ikiendeshwa kama ipasavio kumbe kizuri ni walimu wajuwe namna yakuweza kuongoza kazi zao tu.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 517