homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Morisho Ommy : «Filamu yangu ya Yatima najuwa itagusa wengi sana»

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi kwa Jina la Morisho Gulain Maarufu kama Ommy ni kijana mwenye umri mdogo ila anafanya kazi zakurizisha watu ,hapo ni baada ya kuanzisha company yake iitwayo OMMY THE GREAT FILMS na kuanza Utengenezaji wa Filamu. Pia ni kijana ambaye ameweza kushiriki kwenye Filamu tofauti HAKI na KAFARA, Pia Filamu hizo zimeweza kabisa kutembea sana kimataifa hadi kufanyiwa Promo nchini Tanzania, na nikijana mwenye kujibebea sanaa hata kwenye Comedy pia anashiriki. Apo ni baada ya kuona kazi yake mpya anayo tarajia kuitowa, tumeweza kuwasiliana naye na kumuulizia iyo kazi kijana huyo amefunguka nakusema :

«Kusema ukweli bwana mtangazaji nimekaa mda mrefu sana nikitafuta jina na hapo mwanzo kabisa kabla sijaanza kuigiza nilikuwa nikitafuta group nzuri ambayo itanifunza ndipo nikajiunga na kikundi cha TGF nikaanza kazi na baada ya mimi kuanza kujiona kuwa nimeridhika na mafunzo ndipo niliamuwa sasa kuanzisha group langu kweli nimepata wasanii na nikafanikisha kufanya kazi tofauti tofauti ,na hadi nikatokeya kushiriki baadhi ya Filamu ambazo zimepangwa na wasanii wa kubwa nchini, ila kwa sasa nimeanzisha rasmi company yangu na kwa sasa inafanya kazi na hii kazi ya YATIMA naamini ni kazi nzuri na yenye kutowa mafunzo kwa jamii. Ninacho kiomba ni kwamba Mungu anisaidie nifanikishe ndoti zangu pia wapenzi wakazi za Nyumbani mzidi kunisapoti. »

Alimaliza Ommy uku akisii sana wadhamini wamsaidie ili aweze kutimiza ndoto zake, maana kuna kazi nyingine anatarajia kufanya ,kweli tuzidi kusapoti kazi za nyumbani.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 185