homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Filamu za Burundi kushiriki kwenye RIMA

RIMA maana yake RWANDA INTERNATIONAL MOVIE AWARD ni shirika ambalo linapatikana nchini Rwanda baada yakutoka kuwa National na kwa sasa kuwa international hiyo ni company ambayo imeanza toka mwaka 2012 na hapo washiriki walikuwa ni wa Rwanda tu ila mipango ikaja kugeuka mwaka huu wa 2020 nakutowa matangazo yakupokea kila Movie za nchi tofauti na hapo ndipo baada ya kutangaza Filamu zilizopita pakaonekana pia Filamu za Burundi, moja ya IJWI RY’UMUTIMA iliyotengenezwa na kijana NIPO NIZIGAMA kwenye Category ya Fiction Films, na GENDER QUALITY ambayo inasimamiwa na WISE PRO kwenye Category ya Short films. Basi tulipo wasiliana nao wametuambia :

WISE: “Kusema ukweli tumefurahia sana kwenye Company yetu ya The Brothers kuona Filamu yetu umekubalika kwenye Festival iyo ya Rwanda kwa kweli inatupatia nguvu ila tunaamini kwamba Mambo yatakuwa mazuri tunasubiria iyo siku ya kutowa Tunzo tuone kama tutarudi na Tunzo nyumbani kwa iyo warundi ndugu zetu mzidi kutuombea Mungu tuone kama tutafikisha”. Alimaliza Wise Pro

NIPO NIZIGAMA: “Filamu yangu iitwayo IJWI RY’UMUTIMA nimeshituka sana kwa kweli kuona imepita maana ata mwenyewe nimekuwa sitegemei maana nimeona inavuka inchi sikuwa na amini ila kusema ukweli Filamu Yangu nimekuwa na amini sana kabisa Kweli Mungu asaidie maana nipo pia kwenye category ya kugombania BEST ACTOR Kwa iyo Naamini kwenye Filamu mbili zilizo pita lazima tuje na tunzo tu”. Alimaliza NIPO

Kweli RIMA nchini Rwanda inajitowa kwa kusaidia Filamu za nje na kutambulisha wasanii kimataifa, hapo ni tarehe 7 mwezi March mwaka huu tuombee sana waigizaji wetu.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 40