homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Kube Drama na filamu mpya kwa mara nyingine

Muigizaji pia na mtangazaji nchini Burundi kwa Jina la Kube Drama ambae anazidi kufanya vizuri siku kwa siku kwa sasa imeonekana kujiunga pamoja na company ya KANUMBA THE GREAT FILMS ya nchini Tanzania ambayo kwa sasa ina simamiwa na mama yake mzazi ambae ni Florah Mtegoa pamoja na CAPTAIN HABONA. Hapo ni baada yakujiunga na kufanya kazi kubwa sana ambayo inaonekana kuja na utofauti mkubwa sana kwenye game ya Burundi. Baada ya hapo tuliweza kumtafuta na kumuuliza kuhusu iyo kazi amesema :

“Kusema ukweli naona kama ni nusu ya mafanikio katika Company yangu ya DRAMA FILMS kwa hatuwa hii ambayo nimeanza kuipiga na amini kabisa lazima nitafika mbali pia nashukuru Company ya Jay c Production kunifikisha hapa nilipo saa izi yote kwa sababu ya nguvu yao ndio maana nasema asante sana kwa watu wote wanao nisapoti ,na niwaambie washabiki wangu wamenisapoti sana kwa vile walivyopokeya Filamu yangu ya HOUSE GIRL hadi kwa mwezi mmoja kuvunja record ya views elfu kumi (10K) kweli Mungu awabariki sana naamini pia Filamu mpya inayo itwa SAYARI itakuja kufanya vizuri maana naamini ilo kweli Mungu awabariki na mimi bila nyinyi ni bure sana kabisa ndio maana niseme tu asante, pia mambo mengine ni mazuri naandaa kwa ajili yenu”. Alimaliza Drama

Burundi kwa sasa kuanza kuvuka mipaka ni moja ya hatuwa na mafanikio kwenye kazi yetu kweli Mungu azidi kuwabariki wasanii wetu ili waweze kufika mbali.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 191