homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Skendo : Mimi nasimama upande wote, filamu na comedy

Mchekeshaji wa Filamu nchini Burundi aitwaye Radjabu maarufu kama Skendo Olamide ni mchekeshaji mzuri sana na kazi zake kupendwa zaidi. Ni msani ambae saa hizi ana trend kwenye mtandao wa Niho Tv ambapo comedy zake zinazidi kupendwa. Pia akionekana kwenye upigaji wa picha mzuri na kusema kwamba ni kazi yake umbali na uigizaji. Basi ni baada ya kuwasiliana naye muigizaji huo amesema mengi kuhusu kazi yake :

«Mimi toka nianze mambo ya uigizaji wa filamu kwa sasa takribani miaka zaidi ya kumi (10) na kilichoweza  kunivutia sana ni baada ya kuona wenzangu wanafanya izo kazi nikaanza kujiuliza tu ndani mwangu kama naweza basi nikajaribisha na kweli nikaona naweza ndipo nikaanza mazoezi ya hapa na pale na kweli Mungu akaja kusaidia nikajuwanika na baada ya hapo nilipo kuja kugunduwa ndani mwangu nina talent ya kuchekesha pia ndipo nikaanza sasa kujituma sana na comedy na hapo nikaanza kufanya Show mbali mbali za uchekesheji hadi Mungu akasaidia nikaanza kupata jina ,kweli nawashukuru sana pia watu wa NIHO TV maana wameweza kunisaidia sana hadi napiga hatuwa pia naamini nitafikia malengo tu ,ila tunaomba Watangazaji wa Indundi Tv muendelee kutusaidia ili tuone kama tutafika mahali tunapokwenda. Na washabiki wangu naombeni sapoti zenu ili niweze kufika mbali ». Alimaliza SKENDO

Uchekeshaji una mchango makubwa sana kwenye Tasnia ya Filamu Burundi maana ipo juu sana kuliko Filamu siriazi, kwa hio kubwa zaidi ni waigizaji kujielewa na kufanya ambalo linastaili.

 

What's your reaction?

Related Posts

1 of 510