homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Mtayarishaji na mchezaji wa filamu nchini Burundi kwendelesha kazi zake nje ya nchi

Mtayarishaji wa Filamu pia na Mchezaji wa Filamu nchini Burundi Hakizimana Eshima maarufu kama Eshima ,pia na msimamizi wa Comapany ya ESHIMA VIDEO alikuwa akifanyia kazi zake za filamu nchini Burundi na aliweza kutowa Filamu iitwayo VACANCIER na NAJUTA ambayo alishirikisha wasanii tofauti na Filamu hio kufanyiwa uzinduzi na watu wengi kujitokeza.

Baada ya kwenda nchini Australia aliendeleza Filamu na kwa sasa Filamu zake zinazidi kutamba nchini Australia. Pia tukumbuke anakuwa msanii wa pili nchini Australia ambao wanafanya Filamu uko wenye urai wa Burundi, na kazi zao kuzidi kupendwa.

Basi kwake Eshima kwa sasa yupo pia na kikundi cha uchekeshaji na wanazidi kuvunja rikodi kwa Views za watu kutizama, basi tulipo wasiliana naye kuhusu kazi zake amefunguka na kusema :

“Kweli nina ndoto yakuinuwa Tasnia ya Filamu Burundi na kipaji changu pia ndio maana nilipo badili nchi sikupendelea kuacha Talent yangu kwa kweli basi na ili nikujia vigumu sana kusema nianzishe kikundi hapa ila pole pole nilivyo zoweya nchi nikaanza kupata warafiki na wakafurahia wazo langu ndipo tukaanza sasa kuandaa Filamu na kweli ikatoka watu wakafika wengi sana kwenye uzinduzi kitu ambacho sikutegemea kwa kweli, basi tukaendelesha kazi na pia kinyume na Filamu mimi ni Cameraman pia Editor wa video za wasanii wakuimba Music. Nipendelee kusema tu kwamba washabiki wetu na wapenzi wa Filamu nchini Burundi waendelee kutusapoti siku kwa siku ili na sisi vijana wao ambao tupo nje ya nchi tuweze kupata nguvu yakuendelesha kazi, kweli tunapenda maendeleo ya nchi yetu”. Alimaliza Eshima

Kweli Tasnia ya Filamu Burundi itakuwa na hatuwa kubwa sana maana hapo ni baada ya kijana John K-Ay kufanya vizuri nchini Australia hadi Filamu yake kushiriki shindano ndani ya Hollywood kwa sasa tunatarajia pia mazuri kwa kijana wetu Eshima.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 194