Muigizaji wa kike ajulikanae kwa jina la Belyse Mune ni msichana mwenye uwezo wa kuigiza kila scene na uku akiitendea haki kwa uwezo mkubwa alionao. Pia ni msanii ambae ameshashiriki kwenye Filamu nyingi nchini Burundi kwa Lugha ya taifa pia ni msanii anae jituma sana. Na baada ya ukimya wake tumeamuwa kumtafuta alipo tanganza kwamba anakuja upya kwenye uigizaji wake ,tulipo wasiliana ame sema :
“Kwa kweli ni mda mrefu sana nipo kimya na yote ayo nikutokana na maisha pia nilikuwa kwanza namalizia shule ila baada ya hapo nimefanikisha kweli na nikapata mme nakuolewa yote hayo nisababu yakuweka mazingira sawa, ili nikija kurudi kwenye Game niwe nimekaza kwa usawa, na ivi nimerudi tena kwenye Game na mda tu punde mtaanza shuudia mambo yangu makubwa ambayo nitaanza kufanya. Na kweli kutokana na washabiki wangu wame nimiss sana najuwa ilo ila kuna Saison mpya ambayo inakujia punde tu ambayo inaitwa CHAGUO. Kwa kweli ni nzuri ,na kuna nguvu zaidi ambazo nimetumia kulingana na vile story imenipeleka kwa hiyo najuwa mambo yatakuwa mazuri wasubiri tu”. Alimaliza Belyse
Burundi ni nchi yenye wasanii wakutosha na wenye vipaji ndio maana naomba wasanii waendelee kujitowa na wenye kujitambuwa lazima watafikia malengo.