homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi na kazi yake mpya

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi Mimani Shabani maarufu kama Shabani, ni kiongozi wa Company ya La Colombe Blanche ambayo inafanyia zoezi Bwiza. Pia Shabani ni kijana mwenye kujituma sana kwenye kazi zake, hapo ni baada ya kijana huo kufanya kazi nyingi nakukubalika sana hadi nchini Congo kupokelewa kama mfalme mwaka 2016, kwa kazi zake nzuri anazo endelea kutumika. Basi tulipoona post ya kazi yake mpya tumewasiliana naye ili tuweze kujuwa mengi zaidi amejieleza vyakutosha kuhusu kazi yake nakusema :

“Kusema ukweli hio Filamu yangu ni nzuri sana maana nimetumia na ubunifu wa hali ya juu sana pia isitoshi nimesimamiwa na Director mkubwa sana kutoka Tanzania na ameweza kunisaidia kwa mambo mengi sana hadi kukamilisha Filamu yangu, pia nikumbushe watu kwamba baada ya Filamu yangu ya PENZI LA JENITA sasa nakuja na mabadiliko makubwa sana tena yakushangaza maana mimi naamini kila ninacho kifanya, pia Utaratibu wa Kazi itakavyotoka Mimi nitawajulisha washabiki wangu na wanao fatilia kazi zangu, pia nashukuru sana Indundi Tv kuwa ukaribu wao kwetu sisi waigizaji”. Alimaliza Shabani.

Kwa muonekano wake nikijana ambae anajituma sana nakupambania Filamu za nyumbani kwa kweli maana kwa sasa amekuja na muonekano mkubwa ata kwenye upande wa design.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 191