homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Nyilas, Producer na mtengenezaji mzuri wa Filamu nchini Burundi

Mtayarishaji wa Filamu nchini Burundi Nyilas ni kijana mwenye uwezo mkubwa sana kwenye kazi yake ya utengenezaji wa Filamu na amejichukuliya umaarufu mkubwa sana nchini Tanzania pia na Burundi, hapo ni baada yakuona moja ya kazi aliyo ifanya na kukubalika sana kwenye Trailer ndipo tuliweza kuwasiliana naye na tukamuuliza kuhusu kazi zake na namna alivyoanza, amesema :

“Mimi naitwa Nyilas ndo jina ambalo wengi wanalizowea pia mimi mtanzania ila mama yangu mrundi. Kwanza mimi nimekuwa na ndoto ya kuwa msanii wa kuimba, ila baada ya hapo mimi kuanza kufanya music wa kwanza na wa pili nikaona hakuna mafanikio yoyote ndo nikaamuwa kuanza kuigiza Filamu hapo imekuwa baada ya kurudi Burundi nyumbani nikaanza ila watu wakawa hawatuelewi wengine kutuita wavuta bangi kweli tumekutana na changamoto kubwa sana kabisa. Basi nikarudi tena Tanzania, nikaanza kusoma na baada yakusoma nikarudi tena kwenye Game, ila nikaanza kujifunza ku edit movie na baada ya hapo nilipofanikiwa kujuwa na hadi sasa nafanya kazi zangu vizuri sana na watu wanaanza kutukubali na ndio sasa nipo Burundi na ninajitaidi sana na nimefanya Filamu ya USALITI ambayo itatoka soon hapa na watu wataona kazi zangu na nipo kwa sababu ya wote watakao itaji tufanye kazi”. Alimaliza Nyilas

Kweli ni kijana ambae anazidi kujituma sana kwenye utengenezaji wa Filamu Burundi, na kazi zake anazidi kuzitengeneza nakutendea kila angle ya shoot yake salama na kuonekana bora zaidi.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 518