BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Muigizaji wa filamu Fally aja na umoja wa wasanii

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi Kundu Fally ajulikanae kama Mr Fally, ni mmoja kati ya waigizaji wazuri nchini Burundi -Bujumbura sehemu za Kamenge. Pia alifunguwa kundi yake mwaka 2010 kwa jina la Perfect Vision of Burundi (PVB) na aliweza kutengeneza Filamu na Muigizaji wa Tanzania JEFF ambae alikuwa Actor ndani ya Filamu iliyotamba sana Burundi kwa jina la GAME OF LOVE kwa sasa kijana huyo Fally ameanzisha shirika la wasanii pande za Kamenge nakuitaji umoja ili wafike mbali kwa maendeleo, ndipo tuliwasiliana naye na akasema :

“Kweli Filamu ya Burundi inaitaji umoja bila kujali wewe unajina kiasi gani ,maana ukitazama Tanzania pia kuna BASATA, SHIWABU na BONGO MOVIE zote izo ni shirika za wasanii na ndani utakuta kuna waigizaji wa star tena wakubwa zaidi, kumbe ni vizuri sana ikiwa wasanii tutajiunga kwa pamoja na kutafuta maendeleo, kwa hiyo naomba wasanii wenzangu jikazeni sana tujiunge pamoja ili kutafuta maendelo makubwa, tumeanzisha shirika la wasanii mwaka 2018 ila hatukuweza kufikia malengo kutokana na wasanii kutojielewa, ila naamini kwa sasa wasanii watabadilika kwa hiyo tujitaidi kujenga sanaa ya nyumbani kwa pamoja, maana warundi wanaitaji kazi zetu na washabiki wetu wa nje ya nchi kwa iyo tuungane wasanii wenzangu”. Alimaliza Fally

Shirika inakuwa ni njia moja wapo yakuleta ushirika wa kazi  na maendeleo pia, kama vile ambayo nchi jirani tunakuwa tukisikia, kila kitu mwanzo ni ngumu ila mkijitaidi lazima nifike.

 

Towa Maoni yako…

 

What's your reaction?

Related Posts

1 of 297