BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Filamu ni kipaji changu mimi nimekubalika na kazi zangu zikapendwa now nakuja kivingine

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi Hakizimana Celine ,ni binti aliyekubalika sana kwenye Tasnia ya Filamu Burundi na aliweza kujichukulia umaarufu mkubwa kwa Filamu aliyo icheza iitwayo CHOZI LA MAMA na Filamu hiyo inaweza kushiriki kwenye Shindano nchini Tanzania iitwayo SINEMA ZETU INTERNATIONAL FILM ,na baada ya hapo aliweza kushiriki kwenye Filamu zingine nyingi sana ila baada ya mwaka 2018 alikaa kimya kabisa kwenye Game hadi sasa kutoonekana  ila katika post zake tumeona akisema kwamba anarudi kwenye Game, tulivyo mtafuta alifunguka ma mambo mengi sana akisema :

“Kweli ni mda mrefu sipo kwenye Game ya uchezaji kabisa na yote ayo yamesababishwa na mimi mwenyewe maana tukumbuke kuwa nyuma ya Filamu kuna maisha ambayo mtu anatakiwa kuyaweka sawa ,ndio maana nimekuwa kabisa nimesimamisha kwa miaka 2 yote, ila kipindi kusimamisha nimesikia malalamiko mengi sana pia kwa watu tofauti ,ila mimi mwenyewe ndo nimekuwa najijuwa kabisa na kujuwa niko kwenye nini, maana watu wapo na huwezi kuwakataza kuongea wanachojisikia, ila tu ni waambie kwamba kwa sasa narudi na nitakuja na kazi nzuri tu nina imani mnapenda yes.”

Kweli mwana Dada huu alifanya vizuri sana hadi kufikia kutafutwa kila pande ,kufika hadi Congo nakutengeneza Filamu kutokana na uwezo mkubwa aliyo kuwa nao wa kuigiza.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 308