BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Mugizaji wa Filamu pande za gitega anakuja na mapya

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi ambae anatumikia kazi zake Mkoani Gitega Maarufu kama Muzungu ,kweli nikijana ambae anajituma sana kwa kweli na katika muonekano anajitaidi kutengeneza jina lake vizuri sehemu gitega kwa Filamu za kiswahili pia ni msimamizi wa kundi lake binafsi ,apo ni baada ya kufanya Filamu nyingi tofauti sasa anakuja na mapya na kusema kwamba inabidi atengeneze filamu Bujumbura sasa na filamu hiyo atashirikisha wasanii wenye majina. Tulipo muuliza nini anacho lenga amesema:

«Mimi sijalenga chochote zaidi tu yakuitaji kukuza kipaji changu uku nikiona nikipiga hatuwa,pia ni jambo lakujemga undugu na urafiki kati yetu sisi wasanii wa Gitega na wenzetu apo Bujumbura , maana sote ni watoto wa baba mmoja lazima tuwe na upendo ili tusaidizane kupeperusha bendera yetu kimataifa ,pia naamini kwa kweli tutafika maana apa tulipo tayari tumeshaanza kukubalika inchini kwetu kwa iyo sina mashaka na inje ,ikiwa tu tutajielewa nakufanya lile ambalo linalotakiwa tu lazima tufike kwa kweli,neno moja kwa wasanii wenzangu wote apo Bujumbura na wapenda sana na ninaitani kweli Tuzidi kushirikiana sana ». Alimaliza ivo.

Kweli usifikirii tu kwamba Filamu hoi Bujumbura ata mikoani kuna vijana ambao wanajituma sana kwenye kazi zao ,ila wasanii wakiungana kwa pamoja lazima kabisa wagafika mbali na wataona mabadiliko makubwa sana.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 255