BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Simon Mashakado na kazi mpya iitwayo No Love

Mpambanaji wa Filamu za kiswahili nchini Burundi maarufu Simon Mashakado pia kiongozi na msimamizi wa Company ya MASHAKADO ENT. ,Simon nikijana mwenye umri mdogo sana ,ila hali yake na Tasnia ya Filamu vinakuwa sambamba maana amesema kwamba lazima atimize ahadi yake aliyo ahidi shabiki wake ,na kwa sasa kijana huyo kweli kwenye Tasnia yetu tunakuwa tukimsikia mda kwa mda hapo ni baada ya kuonekana yuko na shoot Filamu ya kifalme kwa sasa anakuja na nyingine. Basi tulimtafuta natukaitaji kuongea naye mawili matatu kuhusu kazi yake amesema :

“Kusema ukweli kuna kitu ambacho kwenye maisha yangu nakuwa naogopa sana nikusema uongo ao kutowa ahadi kisha nishindwe kutimiza, mimi mwaka huu 2020 nimetowa ahadi kubwa kwa washabiki wangu kuhusu kazi zangu na walinitekeleza kwa umakini na walijitowa kunisapoti kutokana na uzinduzi niliokuwa nao, basi namimi lazima niwaoneshe upendo wangu ndio maana kabisa sipati mda wa kulala, kwasasa nikutengeneza Filamu ya Kifalme ambayo kwa mda nitatangaza kuachia ila kwanza kwa kuona nisiwachoshi nimewaandalia Short film nzuri sana iitwayo NO LOVE, ni short film nzuri sana ninayo imani kwamba wataipokea vizuri na siku za usoni tu naachia kazi,kwa hiyo nawapenda sana na endeleeni kuniunga mkono ndugu zangu.” Alimaliza Simon.

Kijana anae jituma na Tasnia ya Filamu akuna ata miezi 6 iliyopita kila siku anajitaidi kukuwa mpya na kuleta mabadiliko katika kazi yake.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 253