BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

“Wa Director wajifunze namna yakufanya Casting nzuri kwa wanawake”

Msanii wa Filamu nchini Burundi kwa jina NAhimana Belyse ni mmoja wa wakina dada wenye kujituma sana kwenye ulimwengu wa Filamu nchini Burundi na kuwa na muonekano tofauti kwa kila kipindi kwenye kazi zake. Dada huyo anaamuwa kusimama na kutetea haki ya wanawake kwenye ujio wa Filamu lazima uzingatiwe maana bila wao Filamu haziendi. Basi tumeongea nae kwa kirefu akasema

“Kweli haki ya mwanamke lazima izingatiwe, nikisema ivo niko namaanisha kwamba wa Director ao zile Team za Casting wajitaidi kuwa wanatendea haki pale wanapo towa role za wadada ,kusema ukweli unakuta story ni nzuri production ni nzuri baadae unaona kwenye Group lako hakuna anae weza kucheza iyo nafasi vizuri ila unakazia kumweka ivo ,kuliko utazame ni dada yupi ambae anawezea ili kazi zako ziende vizuri ,ila kumbuka baada ya wewe kumpa ile nafasi na kuaribu tunachekwa sisi wanawake na kusema kwamba hatujuwi lolote, ila ungejitaidi kumtafuta muhusika na ukampa ata pesa kidogo akaitendea haki Filamu na ikawa nzuri ,kweli mjitaidi sana kubadilika unapofanya Filamu siyo hadi uchezeshe unao waona wewe ila jitaidi sana kupanuwa mipaka kama wenzetu wanavyofanya, na hapo lazima tutafika mbali kwa kweli ,ujumbe wangu unawalenga haswa wa Director pia na zile Team za Casting tujifunze la kufanya kwa kweli ili kuleta eshima ya Tasnia pia na wanawake wetu kukubalika nje”. Alimaliza Belyse

Kweli tunaitaji Burundi pia tupate wasanii wa kike wanaojituma sana na watambulike pia kimataifa kama tunavyo waona wasanii wakike wa nchini jirani.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 543