BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

“Wadhamini wenye TV online waache unafiki wakusema wanatowa sapoti kumbe wanatuangusha”

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi maarufu kama Mr Mvuto kwa jina lake HAKIZIMANA DANNY ,ni msanii mwenye uwezo wakuigiza. Baada yakuongea na Indundi Tv kijana Mvuto ameongea mambo mengi ila ndani yake alikuwa akitowa malalamiko makubwa kuhusu wadhamini wanavyo shindwa kutowa sapoti yaani wao ndo chanzo cha sanaa ya nyumbani kutoendelea kabisa. Basi aliweza kuongea mambo mengi na mazito :

Kusema ukweli ikiwa tutakuwa tunaficha ukweli atuwezi kuendelea,unajuwa Tasnia yetu sisi mama wasanii tunaipeleka vizuri sana tena sana ,ila kinacho tuumiza sisi ni pale unakuta tunatumia nguvu za kutosha ili kazi zetu zifike mbali ila tunakuwa tuna kwama kwa sababu ya uwezo ,ila ukiona wadhamini wengi wanakuja kwa njia ya kujifaidikisha wenyewe ,maana wanakimbilia kufunguwa ma Channel zao kisha wanaanza kututumia sisi kama views zao, yaani unamkuta mtu anakuomba movie yako kisha wanaweka wao kwenye izo Chnanel zao baadae anakuambia kama anakutafutia jina, kusema ukweli tumechoshwa na izo hali,ikiwa wanapenda Filamu yangu na wanataka waweke kwenye Channel yao nazani ni kwasababu nimekodi kamera na pia nikamlipa Editor ,sasa wanapo chukuwa Filamu Yangu Mara moja nakuweka kwenye Channel yao bila kunipa pesa wanafikiria kwamba nitatowa nyingine vipi, kweli waache kuangusha Filamu za nyumbani, wajitaidi waweke sapoti ili tufike mbali maana Burundi pia tunaweza kabisa.” Alimaliza Mvuto

Kweli kijana Mvuto ameshiriki kwenye Filamu za kutosha toka alipoanza Filamu mwaka 2013 hadi sasa ,na alicho kiongea upande mwengine yuko sahihi kabisa maana ikiwa sanaa itakosa uwezo haiwezi kufika mbali, tuungane mkono kwa pamoja lazima mtafika.

Towa Maoni yako.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 544