BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Shemsa: “Mimi ni msanii mpya kwenye Filamu naomba kupokelewa na wenzangu”

Msanii wa Filamu nchini Burundi Shemsa Claudine ,ambae  ni mpya kwenye kizazi cha filamu Burundi ,hapo ni baada ya mda mrefu sana kukaa na kufikiria ataanza aje filamu ila alikuwa anapendelea sana afikie kuwa muigizaji tena mkubwa kabisa ,ila baada ya hapo aliweza kubahatika na kupata kundi lipya. Basi tulipo muuliza ni kitu gani kilicho msukuma hadi kuingia kwenye Filamu amesema:

“Kusema ukweli hakuna mtu aliye nisukuma mimi niweze kuigiza Filamu ila kuna jambo kubwa ambalo nimeligunduwa kwenye maisha yangu ,ikiwa kama Mungu ameweza kumzawadia mtu kipaji ipo siku kinajifunguwaga tu ,kweli mimi ni shabiki wa kutizama filamu za kiswahili ndipo nikaanza kujiuliza ivi kweli mimi nakosa nini ili nianze kuigiza ,basi vilibaki ndani mwangu mda mrefu kabisa ,basi baada ya hapo nilikuwa naenda kutembelea rafiki yangu mara gafla tu kumbe marafiki zangu walikuwa na shooting siku iyo nimekuwa sijuwi lolote,basi hapo ndipo ilikuwa kama vile njia ambayo Mungu amenifungulia nitaweza kuzungumza na viongozi na baadae nikakubaliwa kutokana na vigezo wanavyo viitaji ,basi nikakubaliwa kujiunga. Kweli nina hamu sana ya kuigiza na kuonesha uwezo ambao Mungu aliweza kuweka ndani mwangu naamini kwamba nitafika mbali na ahadi yangu ni kwamba sintokuja kuwaangusha washabiki wangu pia naipenda sana nchi yangu.” Alimaliza ivo Shemsa

Karibu sana kwenye ulimwengu wa Filamu Dada yetu Shemsa maana tunaitaji nguvu zaidi ili kazi za warundi ziweze kufika mbali.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 255